Iowa Congolese Organization and Center for Healing
Shirika la wa kongomani wa Iowa na kituo cha uponyaji
Umuryango w’abakongomani n’ikibanza co gukiriramo
USHUHUDA WETU
Katika mwezi ya tatu mwaka wa 2015 , wakongomani watatu (Boaz, Alex, Safi) walikuwa wameketi kwa apartment moja Urbandale wakizungumuza kuhusu safari yawo kutoka Kongo hadi marekani. Wakati walikuwa wanaongea walijiuliza maswali mawili: je tumufika je Iowa? Ni sababu gani ilisabibisha tukuje hapa Iowa?
Walipi endelea kuongea walikutana wako na kitu ambapo wanachangia wote watatu. Hiyo kitu ni kwamba wawo ni waathirika wa mauaji yalio tokea Gatumba kwenye inchi ya Burundi. Myaka kumi na tatu inayo pita kundi la wauaji limepiga masasi na kuuwa watu kwenye kambi ya Gatumba. Walio kufa wengi ni wakongomani wa kabila la wa Nyamulenge ambao walikuwa wamekimbia vita vilivyo tokea Kivu ya kusini katika inchi ya Kongo. Katika mauaji hayo Boaz amepoteza baba yake na wandugu zake wote, Alex amepoteza baba yake na wadada zake watatu, Safi amepoteza baba yake, mama yake, na wandugu zake watatu. Baada ya myezi sita UNHCR ime anzisha program ya kutafutia watu ukimbizi katika inchi zingine kama America, Canada, Australia, Europe na pengine kwasababu ya kukosa usalama kwa kambi zingine. Mwaka wa 2007 ndiyo wakati waathirika wame anza kuhamishwa kwenye inchi za ukimbizi. Hivyo ndivyo tumefika hapa marekani. Wakati huo hapa Iowa ya katikati kulikuwa wa Kongomani wengine ambao wametoka katika sehemu mbalimbali wakikimbia vita hata wengine wame endelea kuja nyuma.
Baada ya kujiuliza sababu gani tuko marekani, tume amua kuanzisha mradi unao itwa “Kutoka kwenye kifo kwenda kwenye uzima” kama nafasi ya kuanzia huduma zetu. Mradi huu ulikuwa ni kutangaza ushuhuda wetu kwa watu wote jinsi gani tume athirika mauwaji ya Gatumba. Mwezi ya Munane tarehe kumi na tatu mwaka wa elfu mbili na kumi na sita hapa Des Moines, IA ndipo mradi huu umewekwa hadharani kwa usaidizi wa Grand View University, Zion Lutheran Church, na National Home Imporovement. Shabaha ya mradi huu ilikuwa ni kuandika kitabu na kutoa sinema ya ushuhuda wa watu jinsi wame athirika mauaji ya Gatumba.
Mauaji inchini Kongo haja wai kubadhilika. Wafanyakazi wa haki za binadamu watakuambia kuwa ilikuwa ni vile vile. Idadi ya watu waliokimbia inchini Kongo imefikia zaidi ya milioni 2.5. Katika Iowa, ufikaji wa wakimbizi wa Kongo umeongezeka. Kulingana na ofisi kubwa ya umoja wa mataifa kwa wakimbizi, 8,000 mwaka 2013, 13,000 mwaka 2014. Tayari kuna wakimbizi 11,000 wa Kongo ambao walikuwa hapa Iowa tayari, katika kipindi cha miaka 3 hadi 4 ijayo idadi hiyo ongezeka mara tatu. Migogoro inchini Kongo imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu, wakimbizi wengi wa Kongo wamekuwa wakimbizi kwa muda mrefu kama muongo mmoja. Zaidi ya nusu iko chini ya umri wa miaka 17. Sisi ni vijana sana, vijana sana. Tulikuja kutoka mahali ambapo tumekuwa na ukosefu wa elimu kwa sababu ya vita na umaskini. Na elimu tumepata ilikua si kwa lugha ya Kiingereza, kwa hiyo kuna mwelekeo mwingi wa kitamaduni unatakiwa kufanywa wakati tunakuja huku marekani na mahitaji mengi yanahita kuhitajika.
Wakongomani hawaitaji shirika la kuwasaidia tu, bali wanahitaji pia kituo ca uponyaji kwa sababu ya shida wamekumbana nazo za vita, umaskini, mauaji, kubakwa, na kuto kuheshimu haki za binadamu. Katika miaka ya hivi karibuni wakimbizi wengi wa Kongo wame hamishwa Iowa ya katikati kutoka vijijini kwao vilivyo haribishwa na vita kwa msaada wa mashirika kama UNHCR, World Relief, USCRI, Catholic Charities, Lutheran Services na mengineyo. Hii ndiyo sababu ilisababisha sisi kuamua kuwasaida wakongomani wa Iowa ya katikati. Baada ya Boaz kuhitimu kutoka Chuo kikuu alijitolea kuwasaidia wengine akifanya kazi kupitia shirika la AmeriCorps. Huduza zake alizifinyia kwenye shirika la USCRI akisaidia wakimbizi kuwatafutia manyumba na usafiri. Hii ndio wakati Boaz alitambua mahitaji yaliyomo katika wa kongomani wa Iowa ya katikati. Boaz alizungumza na ndugu zake mahitaji yaliopo na tuka amua kuchukua mradi huo kwa ngazi inayofuata kwa kuanzisha shirika ambalo litatumikia jumuiya ya Kongo ya katikati ya Iowa. Mahitaji yalikuwa rahisi kama kusoma barua za kingereza, kuto kujua jinsi ya kulipa bili, usafiri, mawasiliano ya shule na wazazi, kutafsiri, na mengineyo. Timu yetu iligundua kwamba kitu kikubwa kinacho kosekana katika wakongomani "ni watu wakuelekeza wengine." Kutokana na ukosefu wa mwelekezo na shida za lugha watu hawajui kwamba kuna huduma zinazopatikana kwao.
Viongozi wa iCoach ni wakimbizi wa wakongomani ambao wamepitia mambo yote wakimbzi wapya wanapitia kwa sasa na watajitaidi kutumia uzoefu wawo ili wawasaidie wakongomani wenziwe. Wana ufahamu mzuri wa mfumo wa Marekani, wanajua wapi kuna vituo tayari vya rasilimali kuhusu usaidizi wa wakimbizi. Wamoja wetu tumefanya iwezekanavyo hadi kuwa wahitimu wa chuo, wamiliki wa nyumba, na wamiliki wa biashara.
Shirika litatumika kama mwelekezo na kutoa huduma za misaada inayotokana na jamii kulingana na uwezo wake kwa kushirikiana na mashirika mengine yasiyo ya faida ambayo tayari hutoa huduma kwa idadi ya wakimbizi.
OUR TEAM
Boaz Rutekereza Nkingi, Mwanzilishi na Rais
Boaz amezaliwa Vyura Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mwaka wa 2007 ndipo Boaz amekuja marekani na akafikia Saint Louis Missouri kama mkimbizi pamoja na mama yake na wandugu zake wawili. Baada ya Boaz kujua kama kuna watu wa familia yao ambao wameletwa Iowa wote pamoja kama familia tuli amua kuhamia Iowa ili tuwakutane wenzetu kwasababu wao ndio walikuwa wengi. Boaz amemaliza chuo kikuu kutoka Grand View University kwenye eneo la utangazaji wa habari. Tena ako na vyeti viwili kutoka huduma za umma, na mashirika yasio ni ya faida. Boaz amelikwa kwenye maswali ya CW Live TV show na Iowa Public Radio kama mushindi. Boaz ni mshindi wa Iowa College Media Association (ICMA) mara mbili kwa kujua kutunga matangaza ya huduma za umma.
Boaz amekuja marekani kama mkimbizi ambaye anajua kwa kweli ukimbizi ni kitu gani. Ameishi kambini myaka ine kabla akuje marekani. Amekimbia inchi yake kwasababu ya vita iliyo anza mwaka wa 1998. Boaz ako na roho ya kusaidia watu. Anapenda kuimba sana na anapenda kutengeneza vdeo.
Alex Muhire Gatoni, Mratibu wa Vijana
Alex amezaliwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alikuwa na myaka saba wakati alitoka Kongo. Alex alikuja Des Moines, IA mwaka wa 2009 kutoka Bujumbura, Burundi kwenye alikuwa analelewa katika nyumba ya watoto yatima. Amesoma na kumaliza shule ya sekondari hapo Roosevelt High School. Alex hivi ni mwanafunzi kwenye Des Moines Area Community College ambapo ana endelea na masomo ya chuo kikuu. Alex anajihis kuchangia ushuhuda wake na marafiki zake pia watu wote ambao wanapitia mambo ambayo ame mupata. Anapenda kuceza piano, kitari, na ngoma pia anapenda kuceza mpira wa mguu.
Yvonne Munanira, Mtunza hazina
Yvonne Munanira alikuja marekani mwaka wa 2008 pamoja na familia yao. Amesoma shule ya sekondari hapa Iowa na baada aka endelea na masomo kwenye chuo kikuu ca Buena Vista University kwenye eneo la biashara na fedha. Hivi Yyvonne anafanya kazi kama mtaalamu mdogo kwa kampuni moja katika kumpuni kubwa za marekani za bima. Nia yake namba moja ni kuwarudishia mema wale ambao wame mtendea. Mbinu yake ni kufanya kazi moja kwa moja na watu wote. Wakati hana kazi anafurahia kwenda kanisani, kutembea na pia kutumia muda na familia na marafiki.
Eugene Kiruhura, Mtetezi wa familia
Eugene amezaliwa Fizi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lakini alikimbia inchi yake mwaka wa 2004 kwasababu ya vita. Eugene amafika Des Moines kutoka Burundi mwaka wa 2007 na nihapo hapo ameishi mpaka sasa.
Eugene amemaliza shule ya sekondari UVIRA kwa shule la I.S.T.C.E kwenye eneo la fedha, na amefanya mafunzo ya ziada ya kitheolojia tangu kuja hapa Des Moines. Mwaka 2015, Eugene alipokea leseni ya wachungaji kutoka mkutano wa Midwest wa Kanisa la Evangelical Covenant, na kwa sasa anafanya kazi yamasaha machache kwenye Lutheran Services of Iowa kama mkarimani.
Eugene anapenda watu na ana moyo wa huruma kutunza mahitaji ya wengine wakati akiwa mnyenyekevu na mwenye heshima kwa Mungu na watu.
Aline Nkinzingabo, Mtetezi wawa mama
Aline alikuja marekani mwaka wa 2007. Alifikia Abilene, Texas na baadaye akahamia Des Moines, Iowa mwaka wa 2010 ili aishi na wandugu zake. Aline amesoma sekondari Kigali, Rwanda na akapewa diploma tena ni mutu ambae anajitolea sana kuwasaidia wengine kwenye shida zao. Kwa sasa Aline anafanya kazi ya masaha macace kwenye shirika linaitwa Iowa Internation Center kama mukarimani wa Kiswahili, Kirundi, na Kinyarwanda. Anawasaidia tena wazazi ambao hawaongei kingereza kwa sule la watoto hata na hospitali.
Aline akunda gutunganya ahantu hibirori ndetse no kuririmba.